MAJAMBAZI YAPORA MAMILIONI BARCLAYS HABARI KAMILI HII HAPA by nasanyo fortnine

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Camillius Wambura
Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi
wamepora fedha, ambazo thamani yake hazijajulikanakatika Benki ya
Barclays, Tawi la Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Fred Mwezegule, alilieleza NIPASHE jana kuwa watu hao wakiwa kwenye usafiri wa pikipiki, maarufu kama bodaboda, walifika kwenye benki hiyo majira ya saa 3:45 asubuhi.
Alisema waliingia ndani ya benki hiyo kama wateja wa kawaida, huku wakiwa wamemuacha mwenzao mmoja nje kama mwangalizi.
“Walikuja kwenye benki wakiwa wamepakizana, mmoja akiendesha, wawili walishuka na kuingia ndani ya benki. Walivyomaliza kuchukua fedha, mmoja alitoka kashika fuko ninaloamini lilikuwa na fedha na mwingine akiwa na bastola yenye rangi nyeusi na kupiga risasi moja hewani,” alisema.
Alisema tukio hilo lilifanyika ndani ya dakika 10 na baadaye, waliondoka kama watu wanaotoka nyumbani kwao na hawakubugudhiwa na yoyote.
“Wakati wanatoka, mlinzi alijaribu kukabiliana nao. Walimnyang’anya kirungu alichokuwa nacho na kumpiga ngwala na kumwangusha chini,” alisema.
Wafanyakazi wa benki hiyo, ambao mmoja alijeruhiwa kwa risasi kwenye kiganja cha mkono na mwingine alipigwa mweleka na kuanguka chini, walipohojiwa juu ya tukio hilo walikataa kuzungumza.
Meneja wa benki hiyo, ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema hawezi kuzungumzia tukio hilo kwa kuwa siyo msemaji.
Hata hivyo, wateja waliokuwa ndani ya benki hiyo walipoulizwa kama wameporwa fedha, walikana na zaidi wafanyakazi walionekana wakidai kuporwa fedha katika tukio hilo.
Wakati tukio hilo linatokea, mlinzi katika benki hiyo wa Kampuni ya Ultimate Security, alikuwa na kirungu mkononi, huku majambazi hao wakiwa na silaha ya moto.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Camillius Wambura, alifika eneo la tukio nusu saa baada ya kutokea.
Lakini alikataa kuzungumzia tukio hilo na kuwataka waandishi wa habari kumtafuta baadaye.
Hata hivyo, alivyotafutwa kwa simu zaidi ya mara tano, ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni msaidizi wake ambaye alidai Kamanda Wambura anaongea na simu nyingine na baadaye alidai yuko kwenye kikao.

0 comments: