WATANZANIA 15 WANYONGWA HUKO CHINA HABARI KAMILI HII HAPA by tuntu baby

Watanzania 15 wamehukumiwa kunyongwa nchini China baada ya kukutwa na makosa yanayohusiana na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Haule alisema kuwa tangu kuanza kwa kukua kwa kasi kwa biashara haramu ya dawa za kulevya nchini, takwimu zinonyesha kuwa hadi hivi sasa kuna Watanzania 117 wapo katika magereza ya nchini China kutokana na kujihusisha na biashara hiyo.

Alisema kuwa kuanzia mwaka jana, China na Tanzania zimekuwa zikishirikiana katika kuimarisha masuala ya usalama wa nchi hizo mbili hususan katika kupambana na uhalifu wa kimataifa wa pembe na meno ya ndovu pamoja na dawa za kulevya.

Biashara haramu ya dawa za kulevya nchini imekuwa ikikua siku hadi siku pamoja na serikali kuonyesha jitihada za kupambana na tatizo hilo.
 

0 comments:

Copyright © 2014 NASANYO BLOG