ZAIDI YA WAPALESTINA 200 WAFARIKI GAZA HUKU VITA VIKIENDELEA by nasanyo fortnine


Onyo hili linajiri wakati majaribio ya kusitisha mapigano katika eneo hilo la Palestina yakionekana kuti
Maafisa wa jeshi wamesema kuwa
maeneo mengi yanayotumiwa kurusha maroketi kutoka Gaza yamelipuliwa huku
kundi la Hamas likiendeleza mashambulizi ya roketi dhidi ya Israel.
Habari za punde zasema mashambulizi hayo ya
Israeli yamelenga na kupiga nyumba za viongozi wa juu wa Hamas Mahmoud
al-Zahar, na pia ile ya waziri wa zamani wa usalama wa ndani ya nchi
Fathi Hamad.
Mwanamme mmoja mu-Israeli ameripotiwa kufariki
alipogongwa na magruneti ya Hamas alipokuwa amekwenda kuwapelekea
chakula wanajeshi wa Israel walioko karibu na mpaka wa Gaza.Zaidi wa Palestiniana 200 wamefariki katika mashambulio haya ya sasa, wengi wamejeruhiwa, huku majumba na miundombinu ya Gaza ikiwa imeharibiwa sana.
Israel inadai imelazimika kuongeza mashambulio kwani Hamas wamekataa majadiliano ya kidiplomasia.
Hata hivyo msemaji wa Hamas, Osama Hamdan,
ameiambia BBC kuwa hawaiamini Israel na hivyo hawawezi kuzungumzia
mpango wa Amani wanaousikia tu kupitia vyombo vya habari kwani mpango
kama huo hauwezi kamwe kuwasaidia wa- Palestina.Israel inadai imelazimika kuongeza mashambulio kwani Hamas wamekataa majadiliano ya kidiplomasia.
Inasemekana mapendekezo hayo sasa yamewasilishwa rasmi na Hamas wamesema wako tayari kuyajadili.
Mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu huko Gaza yanasema mashambulizi hayo ya Israeli yameharibu hata miundo mbinu ya maji na upungufu mkubwa maji unajiri.
Shirika la umoja wa mataifa la misaada linasema mfumo wa maji machafu haufanyi kazi kamwe na asilimia 90 ya maji yaliyoko si safi kwa matumizi ya binadamu.
0 comments: