WATU 17 WA FAMILIA MOJA WAFARIKI HABARI KAMILI hii hapa by nasanyo fortnine

               Makombora ya Israel yalipua majumba katika eneo la Gaza
  •  
  • Maafisa wa Palestina wanasema kuwa watu kumi na saba wa familia moja wameuawa baada ya makombora ya Israel kuharibu nyumba moja ya ghorofa tatu ya mkuu wa polisi wa Hamas.
  • Tayseer Al-Batsh anadaiwa kujeruhiwa katika shambulizi hilo.


  • Mashambulizi hayo yanajiri baada ya wapiganaji wa Hamas kurusha makombora ya masafa marefu katika miji ya Israel ikiwemo Tel Aviv.
  • Maafisa wa Israel wanasema kuwa makombora mawili ya Roketi yalirushwa kutoka lebanon lakini yakaanguka katika eneo lililo wazi kazkazini mwa Israeli.
  • Na katika hatua ya kulipiza kisasi ,Israel ilirusha makombora nchini Lebanon na kuzidisha hofu kwamba huenda mzozo huo ukapanuka.
  • Takriban raia 150 wa Palestina wameuawa katika mashambulizi hayo huku ikiwa hakuna vifo vyovyote vilivyoripotiwa nchini Israel.

0 comments:

Copyright © 2014 NASANYO BLOG