MBUNGE WA SOMALIA AUAWA HAARI KAMILI HII HAPA by nasanyo fortnine

Mtu mmoja akipekua mabaki katika shambulizi la sokoni huko Hamaerweyne wilaya ya kusini mwa  Mogadishu January 26, 2012. REUTERS/Feisal Omar (SOMALIA - Tags: DISASTER ENVIRONMENT BUSINESS)
Mtu mmoja akipekua mabaki katika shambulizi la sokoni huko Hamaerweyne wilaya ya kusini mwa Mogadishu

Mbunge mmoja wa Somalia ameuwawa katika shambulizi la bunduki linalodaiwa kufanywa na kundi la wanamgambo wa  Alshabab.
Mohamed Mahmud Hayd aliuwawa  alhamisi wakati mtu mwenye silaha alipofyatulia gari lake risasi katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Mbunge mwingine aliyekuwa naye kwenye gari Abdullahi Ahmed Conka aliiambia sauti ya Amerika kwamba washambuliaji hao waliendesha gari lao karibu yake na kufyatua risasi. Anasema mlinzi wa Hayd alijibu kwa  risasi lakini aliuwawa pia.
Afisa mmoja wa bunge kwenye gari hilo alijeruhiwa  wakati Conka alinusurika bila kuumia  .
Al-Shabab yenye mahusiano na Alqaeda ilidai haraka kuhusika na mauaji hayo.

0 comments:

Copyright © 2014 NASANYO BLOG