VIGOGO WA BANDARI WAPANDISHWA MAHAKAMANI LEO by nasanyo fortnine

Aliyekuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA) na Msaidizi wake,
wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
wakikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka.
Washitakiwa hao ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu, Ephraim Mgawe pamoja na aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu, Hamad Koshuma.
Walifikishwa
mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka na Wakili kutoka Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Ben Lincolin akisaidiana na
Wakili wa Serikali, Oswald Tibabyekoma.
Wakili
Lincolin alidai kuwa Desemba 5 mwaka 2011 katika ofisi ya Mamlaka ya
Bandari, washitakiwa wakiwa waajiriwa wa mamlaka hiyo, walitumia vibaya
madaraka yao kwa kusaini mkataba na Kampuni ya China Communication
Contraction.
Ilidaiwa
kuwa washitakiwa hao, walisaini mkataba huo kwa ajili ya ujenzi wa Geti
Namba 13 na 14 katika Bandari ya Dar es Salaam, bila kutangaza zabuni,
jambo ambalo ni kinyume cha sheria na lilikuwa na lengo la kuinufaisha
kampuni ya China.
Washitakiwa
walikana kutenda makosa hayo na kuachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza
masharti ya kusaini hati ya Sh milioni mbili pamoja na kuwa na
wadhamini wawili waliosaini hati ya Sh milioni mbili.
Upande wa mashitaka ulidai upelelezi bado haujakamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 13 mwaka huu, itakapotajwa tena.
0 comments: