MUFTI WA MISRI SHAWKY ALLAM ALAANI WATU WANAOBOMOA MAKABURI YA MITUME HUKO IRAQ by nasanyo fortnine

Ziara la Sheikh Ahmed ar Rifa'i-eneo la Mahlabiya nje ya Mosul likibomolewa na magaidi wa Daesh Ziara la Sheikh Ahmed ar Rifa'i-eneo la Mahlabiya nje ya Mosul likibomolewa na magaidi wa Daesh
Mufti wa Misri Shawky Allam amelaani vitendo vya wanachama wa kundi la kitakfiri la Daesh kushambulia na kubomoa maeneo matukufu walipozikwa Mitume na Maimamu watukufu nchini Iraq, na kwamba vitendo hivyo vinakinzana na mafundisho sahihi ya dini Tukufu ya Kiislamu. Allam amesema kuwa, ni haramu kuwavunjia heshima Mitume na Maimamu watukufu na waja wema kwa kubomoa makaburi yao. Mufti wa Misri ameitaka jamii ya kimataifa kuingilia kati na kuzuia jinai hizo za kuwavunjia heshima watu waliokwishatangulia mbele ya Haki. Amesisitiza kuwa, wanamgambo wa kundi la Daesh wameshindwa kabisa kufahamu mafundisho sahihi ya Uislamu sambamba na kushindwa kusoma historia ya Mtume wa Uislamu Muhammad (SAW). Kwengineko jeshi la Iraq limetangaza kuwa, limeinua bendera katika jingo la ikulu ndogo ya rais katikati mwa mji wa Tikrit nchini humo. Hayo yamethibitishwa na Wizara ya Ulinzi ya Iraq na kuongeza kuwa, mafanikio hayo yamekuja baada ya makundi ya kigaidi kukimbia kufuatia kushindwa na jeshi hilo kwa kushirikiana na vikosi maalumu vya kupambana na ugaidi nchini humo. Kwa mujibu wa wizara hiyo, mapema leo asubuhi jeshi la Iraq serikali na wapiganaji wa kujitolea walianzisha mashambulizi makali ya anga na nchi kavu kwa lengo la kuukomboa mji huo wa Tikrit dhidi ya wapiganaji wa Daesh na kufanikiwa kuyakomboa maeneo mengi ya mji huo sambamba na kuzidhibiti ofisi za serikali na hospitali ya mji huo, huku magaidi wa kitakfiri wa Daesh wakiishia kukimbia na kuelekea maeneo mengine. Wizara ya Ulinzi ya Iraq imesisitiza kuwa hadi sasa operesheni za kuusafisha kikamilifu mji huo na kuwasaka wanachama wa kundi hilo la kigaidi, zingali zinaendelea.
 USISAHAU KU LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK

0 comments:

Copyright © 2014 NASANYO BLOG