TATIZO LA KUTOPATA HAJA KUBWA LASHIKA KASI HABARI KAMILI HII HAPA by nasanyo fortnine
Ni tatizo linalokua kwa kasi kwa sasa kutokana na mfumo wa
maisha yasiyokuwa na mazoezi ya kutosha, vyakula vya kisasa na kuacha
vya asili na pia kuongezeka kwa magonjwa katika jamii mfano kisukari,
kiharusi na kadhalika.
Ni tatizo linalowakumba zaidi wanawake
ikilinganishwa na wanaume. Pia huongezeka kadri umri unavyokwenda.
Karibu asilimia 30 ya watu katika jamii hutumia dawa ili kupata haja
kubwa. Huwa dawa za hospitali au dawa mbadala, tatizo hili huambatana na
kujikamua au kutumia nguvu wakati wa kutoa haja kubwa. Kupata choo mara
moja au mbili kwa wiki, kuhisi choo kugoma kutoka, kupata choo kigumu
au kingi kuliko kawaida, kuhitaji kutumia vidole au njia nyingine ili
kutoa choo kikubwa.
Tatizo hili ni dalili ya magonjwa, ambayo huweza
kuhusu mishipa ya fahamu mfano matatizo katika uti wa mgongo au matatizo
yanayohusu utumbo na mfumo mzima wa chakula, mfano utumbo kupunguza
kasi ya kusukuma chakula au choo, uvimbe katika utumbo n.k. au matatizo
katika kiuno mfano kulegea kwa misuli yake. Pia magonjwa kama kisukari,
kula vyakula vinavyokosa nyuzinyuzi na kadhalika (vya kisasa na visivyo
na mpangilio sahihi). Hii ni kutaja kwa uchache na kwa makundi.
Kwa kuwa tatizo la kupata choo kikubwa kwa shida
ni dalili ya ugonjwa ndani ya mgonjwa bila yeye kuutambua ugonjwa huo,
ni vyema kufanyiwa uchunguzi na vipimo ilikubaini tatizo badala ya
kutumia dawa tu ya kupata choo, kwani hii hutibu tu dalili hiyo kwa muda
huku ikiuficha ugonjwa uliopo na kuupa muda mwafaka wa kuendela kukua
na kuleta madhara makubwa baadaye. Mfano inaweza kuwa saratani katika
njia ya haja kubwa au shida ya mishipa ya fahamu ambayo imeadhirika
kutokana na aina ya kazi, dawa n.k. bila kujitambua au mengine
yaliyotajwa kimafungu hapo juu.
Matibabu ya tatizo hili ni pamoja kuutibu ugonjwa
uliojificha nyuma yake baada ya kugundulika kwa vipimo au uchunguzi,
kuwa na nidhamu katika kula. Pia kubadili mfumo wa vyakula, kunywa maji
ya kutosha na kutumia dawa za kulainisha au kupata choo.
0 comments: