MESSI ,NUER NA JAMES NDIO BORA BRAZIL 2014 WORLD CUP HABARI KAMILI IKO HAPA by nasanyo fortnine


Messi akipokea tuzo la ''Golden Ball''
Lionel Messi, ambaye alipoteza
fursa ya kutwaa kombe la dunia aliambulia tuzo
la mchezaji bora katika
mchuano huo uliokamilika kwa ushindi wa Ujerumani huko
Brazil.
Messi ambaye amesifiwa kwa miondoko yake na
uwezo wake mbele ya lango huko
Barcelona alitawazwa kuwa mchezaji bora
katika mechi nne tofauti.
Messi
alifunga mabao manne katika kipute hicho mbili nyuma ya mshambulizi wa
Colombia James Rodriguez aliyetuzwa kuwa mfungaji mabao mengi mwaka huu.
Kipa wa ugerumani alikuwa na bahati ya kutwaa
nishani ya dhahabu , kombe la
dunia na pia tuzo la kipa nambari moja
katika kipute hicho.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 28 na ambaye
anayeilindia lango mabingwa
wa Ujerumani Bayern Munich aliwapiku mlinda
lango wa Argentina Sergio
Romero na Keylor Navas kutoka Costa Rica.

Nuer akipokea tuzo la ''Golden Glove''
Neuer alifungwa jumla ya mabao 4 pekee katika mchuano huu huko Brazil.
Nuer anachukua wadhfa aliokuwa nao kipa wa Uhispania Iker Casillas.
Mshambulizi wa Colombia James Rodriguez
alitawazwa mshindi wa Golden Boot baada
ya kuongoza katika orodha ya
wafungaji mabao mengi katika mchuano wa mwaka huu
wa kombe la dunia .
Rodriguez alifunga mabao sita akifuatwa kwa karibu na Mshambulizi wa wa Ujerumani
Thomas Mueller akiwa na jumla ya mabao 5.
Licha ya kuwa Colombia iliondolewa katika hatua ya robo fainali Hakuna mshambulizi
aliyeweza kumpiku Rodriguez .

Nuer na Messi walituzwa
Paul Pogba wa Ufaransa alituzwa kuwa mchezaji anayeinukia bora .
Timu ya Colombia ilituzwa kwa kuwa timu yenye nidhamu katika mashindano haya.
0 comments: