MAUAJI YA WANAWAKE VIUNGO VYAO VYATUMIKA KATIKA BIASHARA habari kamili hii hapa by nasanyo fortnine
Mauaji ya wanawake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yameshamiri baada ya
viungo vyao kutumika kama dawa ya kuvutia biashara ya madini na uvuvi.
Uchunguzi uliofanywa katika Mkoa wa Mara umebaini kuwa viungo hivyo vikiwemo sehemu za siri na maziwa ya wanawake hukatwa na kupelekwa kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kutengenezea dawa za kuvuta wateja na utajiri.
imeelezwa kuwa wanawake hao kabla ya kuuawa hubakwa na baadaye hukatwa maungo yao.
Diwani wa kata ya Makoko, mjini Musoma, Aloyce Renatus, alisema kuwa mauaji yaliyotokea katika kata yake, wanawake zaidi ya 10 walikuwa na umri kuanzia miaka 65 hadi 80.
Alisema kuwa mauaji hayo hufanyika kati ya saa 8 mchana na saa 12 asubuhi na wanawake hao huviziwa wakati wakienda mashambani na sehemu ya msitu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Buhare.
“Wanawake wanaouawa ni wale waliokoma hedhi wenye umri kuanzia miaka 65 na 80 kutokana na imani za kishirikina kuwa viungo vyao vinaongeza mvuto wa biashara na kipato kwa wafanyabiashara za madini na wavuvi wa samaki," alisema.
Alisema dawa zinazotokana na viungo hivyo hutumiwa kuwekwa kwenye nyavu za samaki kwa imani kuwa mwanamke ana mvuto,” alisema.
Diwani wa kata ya Buhare Lukas Katikiro, alimweleza Mwandishi wa habari hizi kuwa polisi hawatoi ushirikiano katika kuwakamata watuhumiwa.
Alisema tangu mauaji hayo yaanze hakuna taarifa zozote za kukamatwa watuhumiwa wa mauaji hayo.
Mkazi wa Nyantare, Hellena Chacha (50), alisema mauaji hayo yanawalenga wanawake kwa kuwa hawana nguvu ya kujitetea na mfumo dume uliojengeka kuwa wanawake hawana thamani ya kuishi.
Mfanyabiashara na mvuvi wa samaki, Chales Matiku (28) wa mjini Musoma, alisema kuwa hakuna mfanyabiashara ambaye hatumii dawa za kuongeza kipato kwa kutumia dawa.
Alidai kuwa wafanyabiashara wengi wana imani kuwa wasiotumia dawa hizo hufa mapema au hufilisika kimtaji.
Mganga wa Jadi mjini Musoma, Omary Hassani Abdalah, alimweza Mwandishi wa habari hizi kuwa mwanamke ana mvuto hivyo viungo vyake hutumika kutengeneza dawa ya kuvuta wateja na kuongeza utajiri.
Alisema matiti ya mwanamke hutumika kutengeneza dawa ya kuvuta wateja kwa sababu yanavyotumika kunyonywa na watoto wengi na ndivyo wateja wanavyovutwa katika biashara.
Aidha, alisema sehemu za siri zinasaidia kuvutia biashara za madini kutokana na maumbile yalivyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Paul Kasabago, alisema kuwa polisi wamekuwa na wakati mgumu kukomesha vitendo vya mauaji kutokana na wananchi kutotoa ushirikiano.
Alisema pamoja na polisi kutumia vipimo vya kinasaba (DNA) kuabini ndugu wa marehemu lakini ndugu hao hukataa kutoa ushirikiano.

0 comments: