MACHINGA COMPLEX WAOMBA KITUO CHA BASI by nasanyo fortnine
by nasanyo fortnine
Uongozi wa soko la Machinga Complex jijini Dar es
Salaam, umeiomba serikali kujenga kituo cha daladala katika eneo hilo
ili kunusuru hali ya wafanyabishara wanaoendesha shughuli zao katika
eneo hilo.
Akizungumza jana, Mwenyekiti wa soko hilo, Gerard Mpagama, alisema awali walikutana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Kamati ya Ushauri ya mkoa Dar es Salaam (RCC), halmashauri ya jiji pamoja na ile ya Ilala kama njia mojawapo ya kutatua tatizo.
“Siamini kile kinachoendelea katika soko hili kwa sababu makubaliano yetu hayakuleta matunda, kwa sababu fedha za ujenzi wa kituo cha daladala ziko mikononi mwa manispaa ya Ilala, hivyo kupitia majibu hayo tunaitaka halmashauri ya Ilala kufanya utaratibu haraka wa kupata eneo la kituo,” alisema Mpagama.
Kadhalika alisema sambamba na kituo hicho soko hilo linahitaji eneo la maosheo ya gari, lifti, kwa pamoja vitasaidia kuleta taswira ya soko pamoja na kuongeza idadi ya wachuuzi hasa ukichukulia kuwa wengine ni wazee, na watu wenye ulemavu wa viungo.
Pamoja na hayo, uongozi huo umesema unasikitishwa na dhamira mbaya inayofanywa na baadhi ya wanasiasa ambao wamegeuka kama chambo cha kuzuia kupatikana kwa ufumbuzi wa changamoto za jengo hilo .
“Meya wa manispaa ya Ilala, Jery Silaa, mbunge wa Ilala Azzan Zungu, pamoja na mbunge wa Temeke Abas Mtevu, kwa pamoja wamekuwa kikwazo cha kupinga maamuzi yanayofanywa na watendaji wa mkoa wa kutaka kuupanga mji upya hasa kuzuia uendeshawaji wa biashara maeneo ambayo sio rasmi", alisema.
Katika hilo, alisema Silaa, bila uwoga aliidanganya (Tamisemi), kuwa ameshaziondoa gereji bubu katika eneo hilo ambapo lilitengwa rasmi kama sehemu maalumu ya kituo cha daladala cha machinga complex, wakati anajua fika kuwa zoezi hilo halijafanyika.
“Wakishindwa kufanya hivyo na sisi ni Watanzania wenye haki za kisheria na kikatiba kama walivyo wao, hivyo tutawashtaki kwenye mamlaka husika,” alisisistiza Mpagama.

Machinga Complex

0 comments: