WAZIRI MSAAFU AKATA RUFAA YA ADHABU ALIYOPEWA habari kamili hii hapa by tuntu baby
- Dodoma. Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amekata rufaa
- Kamati Kuu ya CCM kupinga adhabu ya onyo kali aliyopewa na
- chama kutokana na madai ya kuanza kampeni za urais mapema
- kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.
- Akizungumza na gazeti hili mjini Dodoma jana, Sumaye alisema
- kwa ufupi hakuridhishwa na adhabu hiyo na kuthibitisha hilo, tayari
- amekata rufaa.
- Hata hivyo, alisema hadi jana hakuwa amepata mrejesho wowote
- kwa sababu kanuni hazielezi ni muda gani anatakiwa kuwa amepewa
- taarifa kuhusu rufaa hiyo.
- Sumaye na wanachama wenzake, Edward Lowassa, Bernard Membe,
- Stephen Wassira, William Ngeleja na January Makamba walitiwa hatiani
- kwa kuanza kampeni mapema, hivyo kupewa onyo linalokwenda sambamba
- na kutowania nafasi yoyote ndani ya chama kwa miezi 12.
- “Siwezi kuwazungumzia wenzangu, nazungumza kwa upande wangu, sikuridhishwa
- na adhabu hii na nimeshakata rufaa ingawa sijapata majibu yoyote, naendelea kusubiri
- ,” alieleza Sumaye.
- Waziri Sumaye alikataa kuzungumzia hali ya utekelezaji wa adhabu hiyo, akisema
- anachosubiri ni mwitiko wa rufaa yake aliyoiwasilisha Kamati Kuu ya CCM,
- mwanzoni mwa mwezi huu. “Sina kumbukumbu nzuri ilikuwa tarehe ngapi,
- lakini ni mwezi huu wa tatu.”
- Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa juu ya
- rufaa hiyo alisema hana taarifa zaidi ya habari hizo kuzisikia kutoka kwa mwandishi.
- Hata alipotakiwa kueleza nani anatakiwa kuwa na taarifa hizo, alisema: “Mimi ndiye
- msemaji wa chama, hakuna wa kuzungumzia suala hili zaidi yangu. Kwanza inatakiwa
- ijulikane, rufaa hiyo imepelekwa ngazi gani ya uongozi kwa sababu kila ngazi ina muda
- tofauti wa kufanya vikao vyake vya uamuzi.”
- Nnauye baada ya kuelezwa kuwa rufaa ya Sumaye imewasilishwa Kamati Kuu ya CCM
- , alisisitiza kuwa hana taarifa nayo na kwamba haiwezekani rufaa ipelekwe kwenye kikao
- kilichotoa adhabu husika.
- Hata hivyo, Sumaye alisisitiza kuwa rufaa yake ameiwasilisha Kamati Kuu kwa mujibu wa
- kanuni zinazohusika.



0 comments: