VIKOSI VYA CHAD VYAUA WANANE HABARI KAMILI HII HAPA by nasanyo fortnine
by nasanyo fortnine

Vikosi vya Umoja wa Afrika
nchini Jamhuri ya afrika ya kati vinasema kuwa watu wanane wameuawa na
vikosi vya Chad katika mji mkuu wa Bangi.
Vyombo vya habari hatahivyo vimeiweka idadi hiyo kuwa juu zaidi.
Vikosi hivyo ambavyo vilikuwa vimewasili mjini
humo ili kuwatorosha raia wa Chad wanaoishi nchini humo vinadaiwa
kuwafyatulia risasi wakaazi wanaoishi katika maeneo ya wakristo ya mji
wa Bangi.
Chad imeshtumiwa kwa kuwaunga mkono waasi wa kiislamu wa seleka ambao mwaka uliopita waliipindua serikali.
Taifa hilo la Jamhuri ya afrika ya kati limekumbwa na ghasia za kidini tangu kupinduliwa kwa rais Franswa Bozize.
0 comments: