NDUGU WACHARUKA WATAKA KUJUA UKWELI HAWATAKI MASIKHARA by nasanyo fortnine
by nasanyo fortnine

Jamaa kama 30 wa abiria wa
Uchina waliotoweka na ndege ya Malaysia wamesafiri hadi Kualu Lumpur,
mji mkuu wa Malaysia, kuwahimiza wakuu wajibu maswali yao.
Walitoa bango katika uwanja wa ndege wakisema wanataka ushahidi na ukweli kuhusu nini kimesibu ndege hiyo.
Wanataka wakuu wa Malaysia waombe msamaha kwa
kusema kuwa ndege hiyo imepotea katika Bahari Hindi na kwa kuchelewa
kutoa habari hizo.
Mwandishi wa BBC amesema kuwa kuwasili kwao
kulizua hali ya wasiwasi na familia hizo zilipewa ulinzi mkali na watu
wa Malaysia waliojitolea, na hivyo kuwa vigumu kwa waandishi wa habari
kuwafikia.
0 comments: