MGOMO MGOMO HII NI HABARI KAMILI MGOMO WA DALADALA MOROGORO by tuntu baby

MADEREVA wa daladala Manispaa ya Morogoro wamegoma asubuhi hii wakidai
kukamatwa hovyo na matrafiki na hakuna daladala linalofanya safari yoyote katika
manispaa hiyo.
Madereva hao wanadai wameamua kugoma kutokana na kamatakamata ya askari wa
usalama barabarani, ambapo wamesema daladala moja kwa siku linaweza kukamatwa
hadi mara nne na wakihoji wanaambiwa ni makosa tofauti.
Waliongeza kuwa wamepeleka malalamiko yao ngazi mbalimbali za serikali mkoani
Morogoro bila mafanikio.
Mgomo huo umewaathiri zaidi wanafunzi ambao wapo katika mitihani ya nusu muhula
ambapo baadhi yao walilazimika kutembea kwa miguu huku wengine wakirudi nyumbani kujipanga.
Ili kuongeza uzito katika mgomo huo, madereva hao wametoa tahadhari kwa wamiliki
wa mabasi ya Abood kutojaribu kupeleka mabasi yao barabarani kama ambavyo
wamekuwa wakifanya pindi ukitokea mgomo ndani ya manispaa hiyo.......
0 comments: