Polisi wa Kenya wavamia Msikiti wa Musa, Mombasa habari kamili isome hapa by tuntu baby
Watu wawili waliuawa jana na wengine mia moja kutiwa nguvuni
baada ya polisi ya Kenya kuvamia Msikiti wa Musa katika mji wa pwani wa
Mombasa.
Polisi inasema kuwa ilivamia msikiti huo baada ya kupata habari kwamba kunafanyika majlisi inayozungumzia jihadi ndani ya msikiti huo.
Watu walioshuhudia wanasema waliona maiti za watu wawili waliopigwa risasi na polisi na kwamba makumi ya Waislamu waliokuwa katika msikiti huo wametiwa nguvuni.
Polisi inasema ililazimika kutumia gesi ya kutoa machozi baada ya ghasia zilizotokea ndani na nje ya msikiti huo. Polisi inasema Msikiti huo wa Mussa unatumiwa kama kituo cha kueneza fikra na misimamo ya makundi yenye misimamo mikali. Vilevile maafisa wa Kenya wanadai kuwa msikiti huo unatumia kusajili wapiganaji a kundi la al Shabab la Somalia.
Hata hivyo makundi ya kutetea haki za binadamu yameikoa utendaji wa polisi katika tukio hilo. Mkurugenzi Mtendaji wa kundi la kutetea haki za binadamu la Haki Africa lenye makazi yake Mombasa, Khalid Hussein amesema polisi haikuwa na haja ya kutumia nguvu ziada kwa ajili ya kukabiliana na watu waliokuwa msikitini hapo. Hussein amesema polisi ilipaswa kuwa na uvumilivu kwa ajili ya kuzuia umwagaji damu
by tuntu baby

0 comments: