MAUAJI YA KULIPWA HUKO KANDA YA ZIWA WANANCHI WALILALAMIKIA JESHI LA POLISI habari kamili hii hapa....by tuntu baby
bonyeza hii linki...http://www.raiamwema.co.tz/mauaji-ya-kulipwa-yatikisa-kanda-ya-ziwa usome habari kamili tanzania yaangamia....by tuntu baby
WIMBI
la mauaji linaendelea Kanda ya Ziwa ambako maisha ya mtu hupotea kwa
muuaji kulipwa fedha kidogo tu kwa mfano Shilingi laki mbili,
imefahamika.
Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwa mauaji hayo huendeshwa na wakata mapanga ambao hulipwa kiasi cha kati ya Shilingi 200, 000.00 na 1,000,000.00 kutegemeana na ugumu au wepesi wa kupatikana kwa mtu anayetakiwa kuuawa, mazingira na usalama wa mahali anapoishi ama kama ni mwanamke au mwanamume.
Kamanda wa Polisi, aliyepita, wa Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu (sasa Inspekta Jenerali wa Polisi- IGP), aliliambia Raia Mwema kwamba wanafahamu kwamba mauaji hayo ni biashara kubwa.
“ Tumebaini katika uchunguzi wetu kuwa maeneo ya Usukumani, hii ni biashara kubwa. Wako watu wanaishi kwa sababu ya kukata watu mapanga. Wanafahamika, lakini wanaogopwa sana. Hata vilabuni wanakunywa pombe bure,” alisema Kamanda Mangu katika mahojiano yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana kabla ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa IGP mpya akimrithi Said Mwema.
Watu mbalimbali waliozungumza na Raia Mwema wanasema bei hizo za kutoa uhai wa mtu hupanda ama kushuka kama anayetakiwa kuuawa ni mwanamke mzee, kama anaishi peke yake au kwenye mazingira ambayo wauaji wanaweza wasikutane na ugumu wowote, au kama anayelengwa ni mwanamume na anaishi kwenye familia ya watu wengi kiasi gani.
Ni wachache miongoni mwetu ambao tumeshuhudia mtu akiuawa, na bila shaka ni baadhi tu kati ya wachache hao ambao wameshuhudia ndugu zao wakiuawa. Lakini ni wachache sana walioshuhudia mama zao wakiuawa mbele ya macho yao.
Mwajela Maubira (34), mkazi wa Kijiji cha Kwibara, Kata ya Mugango, wilayani Butiama, mkoani Mara, ni miongoni mwa hao wachache walioshuhudia si tu mama yake akiuawa, lakini pia akichinjwa na mwili kuachanishwa na kichwa na wauaji kuondoka na kichwa cha mama yake.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/mauaji-ya-kulipwa-yatikisa-kanda-ya-ziwa#sthash.svoBOuc1.dpufb

0 comments: