YULE ALIYEMUUA MTOTO NA KUMLA UBONGO NAE AMEFARIKI HABARI KAMILI HII HAPA by nasanyo fortnine

Moshi. Yanawezekana yakawa ni moja ya mauaji ya kutisha nchini,
baada ya kijana mmoja kumuua mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya
Msingi ya Marangu Hills Academy kisha kula ubongo wake.
Mbali na kula ubongo wa mtoto huyo, Francis Urassa
(9), mtuhumiwa huyo Lawrence Mramba alijikata sehemu za siri kwa
kutumia wembe na kuzila mithili ya mshikaki akikata kipande kimoja baada
ya kingine.
Hata hivyo, mtuhumiwa huyo naye alifariki dunia
saa chache baadaye baada ya kufikishwa Hospitali ya Kilema iliyopo Moshi
Vijijini wakati madaktari na wauguzi wakimpatia matibabu.
Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea jana saa 1:00
asubuhi Kijiji cha Samanga, Wilaya ya Moshi Vijijini, walidai kijana
huyo alikuwa na nguvu za ajabu lakini baadae polisi walifanikiwa
kumdhibiti.
Wananchi walipiga simu polisi kuomba msaada baada
ya kijana huyo aliyekuwa na panga kuwazidi nguvu na kubakia watazamaji
wakimwangalia namna anavyokula nyama za mwili wake.
Lilikuwa ni tukio lililovuta hisia za wakazi wengi
waliokusanyika kijijini hapo huku wengine wakirekodi tukio la kijana
huyo kula uume wake kwa kutumia simu za mikononi.
Polisi kutoka Mji wa Himo walifika eneo la tukio
na kumkamata kijana huyo wakati huo akiwa katika hali mbaya kutokana na
kupigwa kwa mawe na wananchi na kujikata sehemu mbalimbali.
Mwili wa kijana huyo ulionekana ukiwa umetapakaa
damu kuanzia mdomoni hadi sehemu za siri kutokana na damu nyingi
kuchuruzika wakati akijikata uume vipande vipande na kuula.
RPC Kilimanjaro anena
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz
aliliambia gazeti hili jana kuwa chanzo cha tukio hilo ni upungufu wa
akili uliomkumba kijana huyo na kuanza kuvunja vioo vya nyumba.
“Leo (jana) asubuhi alimkata huyo mtoto wa tajiri
yake kwa panga na kisha na yeye akaanza kujikata sehemu zake za siri na
kula baadaye akajikata pia sehemu mbalimbali za mwili,” alisema.
Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, mtuhumiwa huyo
alifariki katika Hospitali ya Kilema iliyopo Wilaya ya Moshi Vijijini
wakati madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo wakimpatia matibabu.
0 comments: