WAHAMIAJI 19 WAFARIKI HABARI KAMILI HII HAPA by nasanyo fortnine
by nasanyo fortnine

Taarifa kutoka Utaliana
zinaeleza kuwa wafanya kazi za uokozi wamekuta maiti 19 kwenye mashua
iliyowabeba mamia ya wahamiaji kutoka Afrika Kaskazini.
Shirika la habari la Utaliana, ANSA, linasema
inavoelekea wanyonge hao walikosa hewa safi walipogubikwa na moshi wa
injini kongwe chini ya deki.
Wahamiaji wawili kwenye mashua hiyo walinusuriwa kwa helikopta kupelekwa hospitali.
0 comments: