MWALIMU APIGWA MAWE KWA KESI YA KUUA HABARI KAMILI HII HAPA by nasanyo fortnine

Mwalimu wa Shule ya Msingi Chinamili, iliyopo Kijiji na Kata ya Chinamili, Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, amenusurika kifo baada ya kushambuliwa na wananchi kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha mwanafunzi kilichotokea katika kijiji hicho.
Mwalimu huyo, Festo Twange, alivamiwa na wananchi hao wakati akiwa shuleni kwa madai ya kumpiga mwanafunzi huyo wa darasa la tatu, Shilinde Ng’holo (12) kwa madai ya kumpiga. Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Charles Mkumbo, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi, saa 4:00 asubuhi, wakati mwalimu huyo akiwa shuleni akiendelea na majukumu yake ya kikazi.

Alisema mwalimu huyo alinusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa mawe, fimbo, pamoja na mapanga kutoka na wananchi na kumjeruhi na kupoteza fahamu.
Kamanda Mkumbo alisema mwili wake ulikutwa ukiwa chini ya uvungu chumbani kwa shangazi yake.Tayari Jeshi la polisi mkoani hapa linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kuhusika katika tukio hilo, wakiwamo makamanda wa sungusungu, ambao walihusika kwenda kumkamata mwalimu huyo.
Watuhumiwa hao ni Ng’horo Mswahili (34), Luli Malungu (30), Minza Mswahili (48), Sanagula Sali (46), Paul Peter (28), Saba Surwa (15) na Charles Sura (62), ambao wote ni wakulima na wakazi wa kijiji hicho.

Alisema mwanafunzi huyo aliyekuwa akisoma darasa la tatu shuleni hapo, wazazi wake walipoamka asubuhi walikuta akiwa amekwishafariki, huku akiwa uvunguni mwa kitanda.

Kamanda Mkumbo alisema shangazi ya marehemu, Minza Mswahili (48), baada ya kuona mtoto wao amefariki, alienda kuripoti shuleni kwa mwalimu mkuu. Alisema uongozi wa shule ulipopokea taarifa hizo, ulifika eneo la tukio ukiongozana na Minza na kukuta mwili wa marehemu ukiwa chini ya kitanda.

Kamanda Mkumbo alisema baada ya zoezi la kuuona mwili wa marehemu, ghafla Minza alirudi shuleni, huku akipiga mayowe akiomba msaada kwa wananchi kumkamata mwalimu Twange kwa madai ya kusababisha kifo cha mwanaye.

“Baada ya wananchi kusikia yowe, walikusanyika pamoja na wananchi waliokuwa wakipatiwa mafunzo ya mgambo karibu na eneo la shule hiyo nao walikusanyika wakiwa wanaongozwa na kamanda wa sungusungu Magambo Masele akiwa na mtemi wa jeshi hilo, Nkindo Onyashu…waliamua kwenda moja kwa moja shuleni hapo kwa nia ya kumuua mwalimu huyo,” alisema.

0 comments:

Copyright © 2014 NASANYO BLOG