JESHI LA ISRAEL LA AMUA NJIA NYINGINE YA MAPAMBANO GAZA HABARI KAMILI HII HAPA by nasanyo fortnine

Sasa Israel yashambulia Gaza wakitumia vikosi vya angani, ardhini na majini
Israel imeanzisha operesheni ya
nchi kavu pamoja na mashambulizi ya anga na baharini dhidi ya vuguvugu
la kupigania uhuruwa palestina Hamas katika ukanda wa Gaza.
Katika kipindi cha siku kumi zilizopita zaidi ya
wapalestina mia mbili wameuwawa katika mashambulizi ya anga
yaliyotekelezwa na Israel na Muisraeli mmoja aliuwawa katika
mashambulizi ya mizinga ya roketi kutoka Gaza.
Oparesheni hiyo ya kupeleka majeshi ya ardhini imenza usiku, ni operation kubwa kufanywa katika kipindi cha miezi mitano.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema
lengo ni kuharibu kabisa miundo mbinu na silaha zinazotumiwa na
vuguvugu la Hamas kuishambulia Israel.
Vifaru karibu kumi vimeshuhudiwa vikielekezwa
Gaza huku mashambulio ya angani na majini yakiendelea, ripoti ambazo
hazijathibitishwa zinasema huenda hata hospitali zimegwa na mizinga.

Raia wa Gaza walia wakisema hamna pakutorokea huku mashambulizi ya Israel yakiongezeka
Watu zaidi ya 3 wamefariki katika duru hii ya mapigano mbali na wale zaidi ya 200 waliofariki awali.
Kundi la Hamas limesema watajibu oparesheni hiyo
vilivyo lakini Israel inasema Hamas watapewa kipigo cha kudumu na
kitakachowasambaratisha kabisa.
Israel imewaita maelfu ya wanajeshi wake wa akiba kuweka nguvu zaidi katika operation hiyo.
Jana jamii ya kimataifa ilikuwa na matumaini
makubwa kwamba huenda kukawa na usitishwaji mapigano wa kudumu baada
pande zote mbili kukubali mapendekezo ya kusitisha mapigano kwa mda wa
saa 5 za kuruhusu huduma za kibinadamu.
0 comments: