AL-SHABAB WASHAMBULIA TENA IKULU HABARI KAMILI HII HAPA by nasanyo fortnine
Wasomali wakusanyika karibu na mabaki ya gari lililotumiwa kushambulia Ikulu

Wanamgambo wa kundi la kisomali la Al-Shabab washambulia Ikulu ya
rais katika mji mkuui wa Mogadishu siku ya Jumanne magharibi ikiwa ni
shambulio la pili mwaka huu dhidi ya ikulu hiyo.
Maafisa wa Usalama mjini Mogadishu wanasema hakuna ofisa wa serikali
aliyejeruhiwa, lakini wanamgambo na walinzi ni miongoni mwa watu
walouliwa.
Mashahidi wanasema walisikia milipuko mikubwa na milio ya bunduki
kutoka Ikulu ya rais inayojulikana kwa jina la "Villa Somalia", wakati
watu waalipokua wanajitayarisha kufuturu mnamo mwezi huu wa Ramadhan.
Mbunge Hussein Arab Isse ameiambia Sauti ya Amerika kwamba alikua ndani ya jengo la Ikulu wakati shambulio lilipotokea.
"Tulisikia mlipuko mkubwa na kulikuwepo na mapigano
makali kati ya wanajeshi na watu hawa wa Al-Shabab na ilikua inafanyika
nje ya dirisha langu."
Msemaji wa serikali Ridwan Haji ameiambia Idhaa ya Kisomali ya Sauti
ya Amerika kwamba maafisa wote wa vyeo vya juu wako salama na
wanajulikana mahala walipo.
"Rais Hassan sheikh Mohamoud, waziri mkuu na mawaziri
wengine wote, wako salama nilizungumza na waziri mkuu na mawaziri
wengine na wote wako salama."
Waziri wa habari wa Somalia Mustaf Shiekh Ali anasema washambuliaji
wanne wakiwa na bunduki ndani ya gari walijaribu kuingia kwa nguvu ndani
ya uwanja wa Ikulu lakini walizuliwa katika kituo cha ukaguzi. Anasema
washambulizi walilipua bomu ndani ya gari kabla ya kujaribu tena kuingia
katika jengo hilo lenye ofisi za mawaziri kadhaa kwa kutumia nguvu na
mashambulizi ya bunduki.
Waziri Sheikh Ali ameiambia amesema kwamba washambulizi watatu
waliuliwa na dereva kujeruhiwa na anashikiliwa na maafisa wa usalama.
Mkuu wa polisi Kasim Ahmed Roble anasema wanajeshi watatu wa serikali waliuliwa katika shambulio hilo.
Kundi la al shabab limeshadai kuwajibika na shambulio hilo.
Rais Mohamoud akilihutubia taifa Jumanne jioni alikanusha uvumi
kwamba alikimbia kutoka Ikulu. Alisema magaidi wanaweza kueneza madai na
vitisho vyao namna wanavyotaka, kwenye mtandao, lakini hawatofanikiwa
kuwauwa na wale kuweza kuwazuia katika dhamira ya kulilinda taifa.
Afisa wa zamani wa serikali mjini Mogadishu anasema rais alikua
anahudhuria sherehe wakati wa futari katika jengo lenye ulinzi mkali la
uwanja wa ndege.
Hii ni mara ya pili mwaka huu kwa Al-Shabab kujaribu kuushambulia
uwanja wa Ikulu ambako kuna majengo ya serikali na makazi ya baadhi ya
maafisa wa vyeo vya juu.
Katika shambulio la kabla, la mwezi Februarimjitoa mhanga aliendesha
gari lililojaa milipuko na kulilipua kwenye mlango mkuu wa Ikulu na hapo
tena kuzuka kwa mashambulio ya bunduki na kusababisha vifo vya watu
14.
0 comments: