SITA (6) WAUAWA NA MAGAIDI KENYA HABARI KAMILI HII HAPA by tuntu baby
bynasanyo fortnine

Waathiriwa wa shambulizi wakipelekwa hospitalini
Watu sita wameuawa na wengine 25
kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la kigaidi katika eneo la
California mtaa wa Eastleigh, viungani mwa mji wa Nairobi.
Kamanda wa Polisi mjini Nairobi Benson Kibue
amesema kuwa milipuko miwili ilitokea wakati magaidi waliporusha
vilipuzi katika mikahawa miwili midogo.
Mlipuko wa tatu ulitokea katika kituo cha mabasi ya uchukuzi kilichoko karibu na zahanati za afya ya mama na mtoto.
Miongoni mwa waliojeruhiwa walikuwa ni wanawake waliokuwa wanauza mboga na bidhaa zingine za rejareja.
Kwa mujibu wa polisi wale waliouawa walikuwa
wamekwama ndani ya mkahawa huo baada ya mlango kufungwa kutoka nje na
washambulizi waliorusha bomu ndani .
Waathiriwa walikuwa wameenda kununua chakula cha jioni.
Idadi kubwa ya wakimbizi wa kisomali wanaishi katika mtaa wa Eastleigh.
Inaarifiwa washambuliaji walitumia maguruneti au mabomu ya kutengezwa nyumbani kufanya mashambulizi hayo
Mashambulizi haya yanawadia siku moja tu baada
ya mtu anayeshukiwa kuwa gaidi kufa kilipuzi alichokuwa akikiunganisha
kilipolipuka .
Isitoshe wakenya bado wanaomboleza vifo vya
waumini 6 waliouawa katika kanisa moja mjini likoni Mombasa majuma
mawili yaliyopita.
Mtaa wa Eastleigh unafahamika kama ''Mogadishu
ndogo'' kutokana na idadi kubwa ya wasomali wanoishi hapo wengi wakiwa
ni wakimbizi.
Mtaa huu ambao ni kitovu cha biashara umepigwa
darubini na serikali ya Kenya haswa baada ya visa vingi vya ugaidi
kuhusishwa na kundi la wapiganaji wa kiisalmu la Al Shaabab ambao
wamepinga vikali kuweko kwa majeshi ya Kenya nchini Somalia kama sehemu
ya AMISOM.
0 comments: