RAISI ASUSIA MKUTANO HABARI KAMILI HII HAPA by nasanyo fortnine

Maelfu ya waisilamu wametoroka vita CAR na kukimbilia nchi jirani ya CAR
Viongozi wa Ulaya na Afrika
wanatarajiwa kuanza kujadili mgogoro unaotokota katika Jamuhuri ya
Afrika ya Kati, katika mkutano maalum unaofanyika kando na kongamano la
viongozi wa Ulaya mjini Brussels.
Rais Robert Mugabe amesusia kongamano hilo baada ya Muungano wa Ulaya kukataa kumwondolea marufuku ya muda ya Visa mkewe Grace
Bwana Mugabe aliungwa mkono na Rais
wa Afrika Kusini Jacob Zuma, ambaye pia ameamua kuususia mkutano huo
kama ishara ya kumuunga mkono Mugabe.
Zuma alisema kuwa muda umewadia wa Ulaya kukoma kuwaangalia waafrika kama sio watu.
Muungano wa Ulaya tayari umezindua kikosi cha
jeshi lake nchini CAR, na kuelezea mipango yake kutuma wanajeshi 1,000
kuwasaidia wanajeshi wa Afrika na wale wa Ufaransa wanaoshika doria
nchini humo.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa waisilamu 19,000 wanakabiliwa na tisho la kuuawa nchini humo.
Maswala ya Uchumi na Uhamiaji pia yatapewa kipaombele kwenye mkutano huo.
Viongozi 30 wanatarajiwa kuhudhuria kongamano lenyewe wakiwemo marais wa Afrika.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
atahudhuria mkutano kuhusu CAR pamoja na viongozi wa Afrika na wale wa
Muungano wa Ulaya.
Ameahidi kufAnya kila awezalo kuhakikisha anaimarisha juhudi za kukabiliana na migogoro ya kimataifa.
0 comments: