HII NI MAANA HALISI YA PASAKA SOMA UPATE KUFAHAMU by nasanyo fortnine
Maana ya Pasaka kwetu leo. by nasanyo fortnine
Kwetu leo Pasaka inamaanisha mambo mawili. Inamaanisha kwamba kuna njia ambayo
leo tunaweza kupata wokovu. Wanadamu wote ni waovu. Tumezaliwa tukiwa wenye
dhambi na tumeishi maisha ya dhambi. Lakini hii haimaanisha kwamba ni lazima tukufe
katika dhambi zetu. Mungu ametufungulia njia ambayo tunaweza kupata wokovu.
Unaweza kuwa mtu mwovu sana ambaye ameishi maisha yake yote akitumikia dhambi na
uwe hujawahi kuenda kanisani siku hata moja au kufanya jambo lolote zuri. Lakini hii
haimaanishi kwamba hakuna tumaini lolote. Ujumbe wa pasaka ni ujumbe wa tumaini.
Huu ni ujumbe ambao unatueleza kwamba Mungu amefungua njia kwa watenda dhambi
kuja kwake ili waweze kuokoka. Huhitaji kubaki katika dhambi zako, unaweza
kuokolewa.
Pili, Pasaka inamaanisha kwamba wale wote ambao watakuja kwa Kristo Yesu kwa kutubu
na kwa imani, wamehakikishiwa wokovu. Ikiwa utakuja kwa Kristo Yesu leo na uamue
kuacha dhambi zako, ukweli ni kwamba umehakikishiwa msamaha wa dhambi zako nafasi
mbinguni. Ikiwa jutakuja kwake leo na umwombe msamaha wa dhambi zako na maisha ya
milele mbinguni, atakusikia na atakujibu. Huu ndiyo ujumbe wa pasaka. Ni ujumbe wa
tumaini la milele; ni ujumbe kwamba Kristo amaehakikisha wokovu wetu na maisha yetu
ya milele.
Hii ndiyo maana halisi ya Pasaka; ni kifo na kufufuka kwa Kristo na ujumbe wa tumaini
kwa wote ambao wanatafuta wokovu.
“Kwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye
umuhimu wa kwanza: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu,
kama yasemavyo maandiko, ya kuwa alizikwa na alifufuka siku tatu” (1
Wakorintho 15:3-4).
Katika kifungu hiki cha Bibloia mtume Paulo anatueleza kuhusu ujumbe mkuu wa Biblia.
Anatuonyesha kwamba katika Biblia kuna mambo ambayo ni yanafaa kupewa umuhimu
zaidi. Tunasoma kuhusu mambo haya bi gani. Kwa hivyo Biblia hatufunzi tu kuhusu
ujumbe muhimu wa Biblia, bali pia inatufunza pasaka ni nini. Kifungu hiki kinatueleza
kwa nini ujumbe wa Biblia ni wa muhimu sana na ni kwa nini tunafaa kuuelewa vyema
sana na kuupokea kwa mioyo yetu yote.
1. Pasaka inahusu kifo cha Bwana Yesu Kristo.
Biblia inasema katika kifungu hiki kwamba, “Kwa maana yale niliyopokea ndiyo
niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya
dhambi zetu, kama yasemavyo maandiko.” Hii inamaanisha kwamba kifo cha Kristo Yesu
ndiyo tokeo la muhimu sana katika historia ya ulimwengu wote. Wakati tunasoma Biblia
lazima tufahamu kwamba msingi wake wote ni kifo cha Yesu Kristo.
2. Pasaka inahusu kufufuka kwa Bwana Yesu Kristo.
Biblia inasema katika kifungu hiki kwamba, “Kwa maana yale niliyopokea ndiyo
niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya
dhambi zetu, kama isemavyo maandiko, ya kuwa alizikwa na alifufuka siku ya tatu” (1
Wakorintho 15:3-4).
Lazima tukumbuke kwamba Agano la Kale lote linatuongoza kwamba Kristo Yesu na kifo
chake. Tukumbuke kwamba waandishi wa Mathayo, Marko, Luka na Yohana, wakati
waliandika vitabu hivi, waliandika wakituongoza kwa hili tokea moja, yaani kifo cha
Bwana Yesu Kristo. Kila sura ya vitabu hivi vine vya injili, inatuongoza kwa msalaba wa
kristo Yesu. Nyaraka za mitume wote msingi wake ni kifo cha Kristo Yesu. Ni kifo cha
Kristo Yesu ambacho kiliwaongoza kuandika ujumbe ambao waliandika. Kifo cha Kristo
Yesu ndiyo tokeo la maana kabisa.
Katika kifungu hiki tunaelezwa kwamba kifo cha Kristo kiilikuwa kimetabiriwa katika
maandiko. Hii inamaanisha kwamba Agano la Kale lote linazungumzia kifo cha Kristo
Yesu kama tokeo kuu katika historia ya ulimwengu wote. Hili ni tokeo ambalo lilitabiriwa
kwa njia tofauti tofauti katika karne zote. Hili ndilo tokea ambalo Mungu alizungumza
kuhusu wakati alimwambia Shetani kwamba, “Atakuponda kichwa, nawe utamgonga
kisigino” (Mwanzo 3:15). Hili ndilo tokea ambalo Mungu alikuwa anakudia wakati
aliwamuru Waisraeli watoke dhabihu za wanyama katika hekalu. Sheria ya Musa
ilitayarisha njia ya kuja kwa kristo Yesu na kifo chake.
Sababu kwa nini kifo cha Kristo Yesu ni cha maana sana ni, kwa sababu kupitia kwa kifo
chake, wanadamu waokolewa kutoka kwa dhambi zao. Biblia inasema, “Kristo Yesu
alikuja ulimwenguni kuokoa wenye dhambi” (1 Timothy 1:15). Hili ndilo likuwa kusdi la
Kristo kuja hapa ulimwenguni: kuwaokoa wenye dhambi kutokana na hatia na uchafu wa
dhambi. Kifo chake na kufufuka kwake ndiyo njia ambayo inatuletea wokovu na
kutuingiza mbinguni. Bila kifo na kufufuka kwa Kristo Yesu, hakuna wokovu kwa mtu
yeyote. Hii ndiyo njia ambayo Mungu ameweka ili sisi tupate kuokoka na ndiyo njia
ambayo tunafaa kutumiikiwa tunataka kuokoka.
Ikiwa hujaokoka, utabaki katika dhambi zako hadi utakapokuja kwa Kristo Yesu kwa
kumwamini. Utabaki ukiwa hujaokoka hadi utakapoamini katika kifo na kufufuka kwake.
Lazima umwombe Mungu akusamehe dhambi zako zote kupitia kwa kifo cha Kristo Yesu
msalabani kalvari. Hii ndiyo njia ya pekee ya kupokea msamaha wa dhambi zako, yaani
kupitia kwa kifo cha Kristo Yesu msalabani.
Kama tu vile kifo cha Kristo Yesu ndiyo msingi wa ujumbe wa injili, vivyo hivyo pia
ndivyo ilivyo hata kufufuka kwake. Paulo aliwafundisha Wakorintho kuhusu kifo na
kufufuka kwa Kristo Yesu kwa sababu alijua kwamba mambo haya ndiyo msingi wa
ujumbe wa injili.
Kufufuka kwa Bwana Yesu Kristo kunamaanisha kwamba Mungu alikubali dhabihu ya
Kristo kwa ajili ya watenda dhambi. Msalabani Kalvari Kristo alijitoa kwa ajili ya watenda
dhambi na damu yake ili iweze kuwaosha wenye dhambi kutoka kwa dhambi zao. Hivi
ndivyo Bwana Yesu kristo alikuwa anafanya msalabani. Alikuwa anafanya kile ambacho
makuhani wa Agano la Kale walikuwa wanafanya wakati waliwatoa wanyama kama
dhabihu kwa ajili ya watu wote. Walitoa wanayama ambao walikuwa hai ili watu wa
Isreali wasihukumiwe na Mungu. Pia walitoa damu ili watu waweze kuoshwa kutoka kwa
dhambi zao.
Hivi ndivyo Bwana Yesu Kristo alifanya msalabani Kalvari kwa ajili ya watenda dhambi.
Alitoa maisha yake kwa ajili ya dhambi zao na damu yake ili waweze kuoshwa dhambi
zao. Kwa hivyo, tunajua kwamba Mungu Baba alikubali dhabihu ya Kristo kwa sababu
alimfufua kutoka kwa wafu. Kwa kumfufua kutoka kwa wafu, Mungu Baba alikuwa
anasema kwamba yeyote ambaye atamwamini Kristo kwa ajili ya wokovu wake,
ataokolewa kutoka katika dhambi zake na kuhakikishiwa nafasi mbinguni. Kwa sababu
Kristo Yesu alifufuka, ako na uwezo wa kuwaokoa wote ambao wanakuja kwa Mungu
kupitia Yeye (Waebrania 7:25).
Kwa sababu Kristo Yesu alifufuka, ni dhihirisho kwamba Yeye pekee ndiye njia ya
wokovu kwa watenda dhambi. Wakati Mungu Baba alimfufua Kristo kutoka kwa wafu,
alikuwa anasema kwamba, ni wale tu ambao wanakuja kwake kupitia kwa Kristo ndiyo
wataokoka. Kwa sababu ni Yeye ambaye Mungu amempa mamlaka ya kuokoa. Kuna
watu wakuu ambao huwapataia watu Fulani mamlaka na husema kwamba ikiwa mtu
yeyote anataka kuwaona, lazima mtu apitie kwa mtu au watu hao. Ikiwa mtu hatapitia
katika mtu huyu, basi hataweza kumwona mkuu huyo. Kristo ndiye amewekwa na Mungu
kuwa Mwokozi wa ulimwengu. Tunajua hili kwa sababu Kristo ndiye amefufuliwa na
Mungu. Kufufuka kwa Kristo Yesu si kama kule kwa Lazaro. Lazaro hakupewa mwili
mpya ambao haungekufa tena. Baada ya miaka michache baada ya Lazaro kuregeshewa
uhai, alikufa tena. Lazaro hauko hai leo katika mwili mpya.
ASANTE KAMA UNA MAONI USHURI TUMA TEXT KWA NAMBA HII +255 767 361 980 AU COMMENT HAPO CHINI
0 comments: