POLISI DAR AIBA MTOTO MBEYA HABARI KAMILI HII HAPA by nasanyo fortnine


by nasanyo fortnine
Polisi wa kike anayefanya kazi Kituo cha Polisi Ilala,
Dar es Salaam amekamatwa jijini Mbeya kwa tuhuma za kuiba mtoto mchanga
wa siku saba, Goodluck Salehe wilayani Kyela.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya, Ahmed Msangi alisema mtuhumiwa alikamatwa juzi saa 4 asubuhi
eneo la Meta akiwa na mtoto huyo.
“Ni kweli tumemkamata askari wa Kituo cha Polisi
Ilala, Dar es Salaam akiwa na mtoto aliyeripotiwa kuibwa Aprili 6, mwaka
huu wilayani Kyela,” alisema Msangi.
Akifafnua alisema mtoto aliyeibwa alizaliwa Machi 30, mwaka huu na kupotea katika mazingira ya utatanishi Aprili 6, mwaka huu.
Akifafanua kuhusu tukio la wizi, alisema mama wa
mtoto anayeitwa Mboka Mwakikagile akiwa Kitongoji cha Sama A Kijiji cha
Ibanda Kata ya Itope, Kyela alipigiwa simu na mwanaume ambaye mzazi
mwezake anayeishi Kasumulu kwamba atafika shangazi wa mtoto kuwaona na
ampokee na waende hospitali.
Alisema baada ya muda, Mwakikagile akiwa nyumbani
kwa wazazi wake alimpokea mwanamke aliyejitambulisha kuwa ni dada ya
mzazi mwenzake akiwa na begi la nguzo za watoto.
Baada ya mazungumzo, mwanamke huyo alimshauri
Mboka kumpeleka mtoto huyo kliniki ili akapate matibabu ya kinga jambo,
ambalo mama wa mtoto aliliafiki.
Mama wa mtoto anasema yeye na yule mwanamke
waliondoka kwenda Zahanati ya Njisi Kasumulu na walipofika waliambiwa
kununua daftari kwa ajili ya mtoto.
Alisema alikwenda kununua daftari na aliporejea
hakumwona mwanamke aliyemwachia mtoto wake na alipouliza aliambiwa
ameondoka na pikipiki.
Kamanda Msangi alisema uchunguzi wa awali unaonyesha mtuhumiwa huyo alikula njama na baba mzazi wa mtoto huyo ili kufanikisha.
Msangi alisema taratibu zinafanyika kumfungulia mashtaka na kisha kufikisha mahakamani.
0 comments: