AVIMBA UVIMBE WA AJABU MDOMONI AOMBA MSAADA JIONEE MWENYEWE by tuntu baby


Hali aliyonayo Asha Manga.
Akizungumza Asha alisema: “Nikiwa kidato cha nne ndipo
hili tatizo liliponianza, nilihisi ni jipu lakini kadiri siku
zilivyosogea, uvimbe uliongezeka.
“Nilikwenda Hospitali ya Wilaya ya Turiani nikafanyiwa uchunguzi na kupewa dawa, nikapata nafuu na kuendelea na masomo.
“Mwaka 2008 hali ilinirudia tena nikashindwa kuendelea na masomo
yangu ya kidato cha tano. Nilikwenda hospitali ambapo daktari
alinichunguza na kunipatia dawa lakini sikupata nafuu.
“Nilirudi pale hospitalini ambapo daktari aliniambia natakiwa
kufanyiwa matibabu ya haraka kwani naweza kupata tatizo la saratani.
“Nilipoambiwa hivyo, nililia sana kwani nilijua mwisho wa maisha
yangu umefika kwa sababu mimi na mama yangu ni maskini, maisha yetu
magumu… hata kula yetu ni ya shida.”
Asha anaeleza kuwa, baada ya kuambiwa hivyo alifikishwa katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa msaada wa Mkurugenzi wa Asasi ya
Wezesha ya Morogoro, Lusako Mwakiluma, ikabainika taya lake limeharibika
na zinatakiwa shilingi milioni 4 ili awekewe lingine.
Msomaji wetu, Asha anahitaji msaada wako ili apone hivyo unaweza kuchangia chochote kupita namba 0713 33 74 49, 0767 44 81 86 au akaunti namba 01 52 39 29 51 2000 ya CRDB.
0 comments: