WATU 20 WAUAWA KATIKA SHAMBULIO HABARI KAMILI HII HAPA by nasanyo fortnine
Watu 20 wauawa katika shambulio la guruneti CAR by nasanyo fortnine
Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangaza kuwa, watu 20
wameuawa katika shambulio la guruneti lililoulenga mkusanyiko wa watu
waliokuwa katika mazishi mjini Bangui, nchini humo. Hayo yamethibitishwa
na Wizara ya Usalama wa Jamii nchini humo na kuongeza kuwa, serikali
inalaani vikali shambulizi hilo na imetaka kufanyike uchunguzi wa haraka
ili kuwabaini wahusika wa jinai hiyo na kuwapandisha kizimbani.
Shambulizi hilo limetokea katika hali ambayo Shirika la Kuhudumia
Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeonya kuwa, askari wa kimataifa
wa kulinda amani nchini humo, ndio tu wanaoweza kutoa ulinzi kwa
Waislamu wanaoendelea kushambuliwa na wanamgambo wa Kikristo wa
Anti-Balaka ambao Umoja wa Afrika umewatangaza rasmi kuwa ni magaidi.
Volker Turk mmoja wa viongozi wa shirika hilo ambaye ametoka nchini
Jamhuri ya Afrika ya Kati hivi karibuni, amesema kuwa, kiwango cha chuki
za kidini kilichopo nchini humo, kinatia wasi wasi mkubwa. Ameongeza
kuwa, kuna tishio kubwa la kumalizika Waislamu katika mauaji
yanayofanywa na Anti-Balaka na ametaka kuchukuliwe hatua kali za
kukabiliana na wimbi hilo la ukatili na mauaji hayo.
0 comments: