POLISI WANNE WATIMULIWA KAZI HABARI KAMILI HII HAPA by tuntu baby

Kamishna Suleimani Kova

Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam limewafukuza kazi askari  polisi wanne  kwa makosa ya kuhusika katika uhalifu.

Askari hao ni Rajab Mkwenda mwenye namba E 6396 wa polisi makao makuu, Saimon  F 9412 wa kituo cha kati, Albas Poosa F 9414 wa bendi ya polisi Dar  na Suleiman  F 9512 wa Kigamboni.  

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleimani Kova alisema askari hao wamekuwa wakihusika katika uhalifu ikiwa ni pamoja na tukio la majambazi 15 waliovamia kampuni ya Kichina ya Hong Yang iliyopo Mbezi Beach A.

“Hatua iliyochukuliwa na polisi kuwafukuzwa kwa fedheha inawastahili kutokana na kulidhalilisha Jeshi la Polisi  na wamefukuzwa kazi kuanzia tarehe 17 Machi  na hatutavumilia vitendo vya ukiukwaji wa maadili” alizema Kamishina Kova.

Alisema majambazi hao walipora vitu mbalimbali ikiwemo simu na fedha  na kugundulika kuwa baadhi ya majambazi hao ni askari polisi ambao nao walishiriki katika tukio hilo.

Kova aliongeza kuuwa, jalada la kesi hiyo pamoja na majalada mengne yatapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kabla ya kuwafikisha mahakamani askari hao kwa makosa ya jinai.

Katika hatua nyingine, Kamishna Kova alisema wamefanikiwa kukamata tindikali lita 21 maeneo ya Vingunguti Miembei wilayani Ilala katika chumba cha mkazi mmoja wa eneo hilo ambaye hakuwapo chumbani wakati huo na upelelezi unaendelea ili kumtambua na kumkamata

0 comments:

Copyright © 2014 NASANYO BLOG