POLISI IRINGA WAPEWA SIKU SABA NA CCM HABARI KAMILI HII HAPA by tuntu baby

Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa kimempa siku saba Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Iringa, Sifael Pyuza kuomba radhi chama hicho kutokana na polisi kufanya msako chumba hadi chumba kwenye jengo la makao makuu ya CCM mkoani humo kwa madai  ya kuwa chama hicho kiliwateka baadhi ya
 vijana wa Chadema na kuwatesa katika jengo hilo siku ya uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga
 alisema siku ya uchaguzi huo uliofanyika Jumapili iliyopita, mkuu huyo wa polisi wilaya ya Iringa aliongoza upekuzi katika jengo hilo kwa madai kuwa chama hicho kiliwateka na kuwashikilia baadhi ya vijana wa Chadema katika jengo hilo jambo ambalo si la kweli.

 "OCD alikuja hapa ofisini akiwa na vijana wake wametupekua chumba hadi chumba, hii ni unyanyasaji na udhalilishaji kwa chama, sisi ni chama tawala hatuwezi kufanya vitendo vya kihuni kama hivyo vinavyodaiwa" alisema Mtenga.

Alipoulizwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi kuhusiana na malalamiko hayo, alikiri kumuagiza Mkuu huyo wa polisi wilaya kufanya upekuzi katika jengo la makao makuu ya CCM mkoa wa Iringa baada ya kupata taarifa kutoka Mkururugenzi wa Oganizasheni za Chadema, Bensoni Kigaila kuwa kuna wafuasi wa chama hicho wanashikiliwa na kuteswa katika jengo hilo.

 "Nilimtuma OCD wangu kufanya msako jengo hilo chumba hadi chumba ili kubaini kama kweli kuna watu waliotekwa na kunyanyaswa lakini baada ya kufanya msako nililetewa mrejesho kuwa hakuna vijana wa Chadema waliotekwa na kunyanyaswa" alisema Kamanda Mungi.

0 comments:

Copyright © 2014 NASANYO BLOG