HICHO NDICHO ALICHOSEMA SPIKA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI by nasanyo fortnine

Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA), Dk. Margareth Ziwa.
Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EALA), Dk. Margareth Ziwa amesema juhudi kubwa zinahitajika kufanywa na
nchi wanachama kurekebisha sheria zao ili ziweze kuendana na kuimarisha
nguzo za mtangamano ya jumuiya hiyo.
Alitoa changamoto hiyo juzi baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambaye pia ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kulihutubia Bunge hilo kwenye makao makuu ya jumuiya jijini hapa.
Dk. Zziwa alitaka kwa mfano, Mkataba wa Soko la Pamoja (CMP) ambao ulisainiwa na nchi wanachama miaka minne iliyopita, unaelezea kuhusu faida ambazo jumuiya hiyo inaweza kupata kama vile wakazi wake kutembelea nchi yoyote mwanachama bila vikwazo, wafanyakazi, huduma na usafirishaji wa bidhaa huru na mambo mengine.
“Bado hatujaona utekelezaji wake kwa nchi wanachama lakini tuna imani kwamba zinaweza kutekeleza kwa kuwa zipo katika hatua mbalimbali kurekebisha sheria zao ili ziweze kuendana na CMP, hata hivyo, tunaomba mchakato wa kisheria uweze kuharakishwa,” alisema.
Alipongeza nchi wanachama kusaini Mkataba wa Umoja wa Sarafu ya Fedha wa Novemba 2013, kwa kusema wananchi wa nchi husika watapata faida kubwa kwani ushindani utakuwapo.

usisite kulike page hii
0 comments: