BAADA YA NDEGE KUTOONEKANA KABISA MAREKANI YAAMUA HIVI habari kamili hii hapa by tuntu baby

by tuntu baby

Juhudi zimeelekezwa sasa katika Bahari Hindi
Marekani imetuma vikundi vya watalaamu katika bahari Hindi kusaidia katika juhudi za kuisaka ndege ya Malaysia iliyotoweka, baada ya madai kuibuka kuwa huenda ndege hiyo iliendelea kupaa kwa zaidi ya muda ambao wachunguzi walidhania hapo awali.
Maafisa ambao hawakutaka kutajwa wanasema kuwa ndege hiyo ilituma data ya Satelite kwa zaidi ya saa tano baada ya kutoweka.
Hata hivyo wachunguzi walisema data hiyo ya Satelite haijaelezwa kwa kina ingawa serikali ya Malaysia imekanusha madai hayo.
Vyombo vya habari vya serikali ya China vinadokeza kuwa wataalam wanasema huenda ndege hio ilianguka katika ziwa la kusini mwa Nchi hiyo .
Hata hivyo maafisa wa Marekani wanaosaidia katika upelelezi huo wanasema kuwa huenda ndege hiyo ilikuwa ikituma mawasiliano kwa Satelite hata baada ya kutoweka Jumamosi na kwa hivyo wanaelekeza juhudi zao Magharibi mwa bahari hindi.
Afisa mkuu wa mauzo wa shirika hilo la ndege Hugh Dunleavy amepuuzilia mbali ripoti hizo.
Serikali imesema kuwa msako wa ndege hiyo utaendelea hadi eneo la Magharibi katika bahari Hindi.
Waziri wa usafiri, (Hishammuddin Hussein) amekataa kuzungumzia ripoti za Marekani kuwa Ndege hiyo iliendelea kupaa kwa saa kadhaa kabla ya kutoweka.
Mkuu wa Halmashauri ya usafiri wa ndege nchini Malaysia, (Azharuddin Abdul Rahman) amesema kuwa Malaysia inashirikiana na Marekani kubaini ikiwa kuna taarifa zozote za Satelite ambazo zinaweza kusema iliko ndege hiyo iliyotoweka ikiwa imebeba watu 239.

0 comments:

Copyright © 2014 NASANYO BLOG