ACHOMWA MOTO KWA WIZI WA PIKIPIKI habari kamili hii hapa jisomee by tuntu baby

Kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mapema hii leo akamatwa huko maeneo ya kihonda na kushushiwa kipigo kizito na kuchomwa moto....
kijana huyo inasadikika aliiba pikipiki miezi kadhaa nyuma na kutokomea kusikojulikana na kama ilivyo desturi ya kuwa mungu hamtupi mja wake baada ya kuiba na kufanikiwa kuuza leo hii ajichanganya na kuonekana tena maeneo ya yule aliyemwibia na kusababisha kukumbana na kisanga hicho cha kuchomwa moto alishushiwa kipigo cha kufa mtu na kuulizwa wapi ilipo pikipiki awali alitaja maeneo ya karibu na  wilaya ya mvomero..(mpasha habari anaendelea kusema) bila hiyana bodaboda wakajikusanya na kuondoka nae mpaka hapo alipotaja alipokuwa karibu ya kufika akabidili maamuzi na kusema kuwa pikipiki hiyo haipo hapo ipo dumila hapo ndipo alipowapandisha hasira bodaboda hao walioenda nae (mpasha habari anaendelea kusema) kuwa bodaboda hao waliamua kucharuka na kuanza tena kipigo ambacho kilipelekea kuamua kumchoma moto kabisa wakitumia makoti yao waliyoyavaa na mafuta ya petroli waliyonayo kwenye piki piki zao mpaka pale walipohakikisha amebaki mizoga wakaamua kuondoka huku wakisema fundisho kwa wengine

kwa bahati mbaya hakuweza kuchukua picha kwa kuwa hakuwa na simu yenye kamera harafu isitoshe anasema tukio lilikuwa lakutisha sana

unachukuliaje uamuzi huo toa maoni yako hapa chini;;;...

0 comments:

Copyright © 2014 NASANYO BLOG