MADAWA YA KULEVYA YAKAMATWA HUKO ZANZIBAR habari kamili isome hapa by tuntu baby
by tuntu baby
Kamanda Nzowa amesema dawa hizo za kulevya zimekamatwa na Polisi wa doria baharini muda wa saa sita usiku wa kuamkia Jumanne zikisafirishwa katika Jahazi.
Kwa mujibu wa Kamanda Nzowa Shehena hiyo ilikuwa ikitoka nchini Iran kuelekea nchi au eneo ambalo mpaka sasa bado halijafahamika.
Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya kukamata dawa za kulevya aina mbalimbali kupitia viwanja vya ndege,nchi kavu na baharini, ambapo mwaka jana kiasi kikubwa cha dawa za kulevya zilizokamatwa ziliteketezwa

Dawa ya kulevya aina ya Heroine na bomba la sindano
Polisi nchini Tanzania
wamekamata shehena ya dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa kilo
201 katika eneo la bahari kati ya Dar es Salaam na Zanzibar nchini
humo.
Kamanda wa kikosi maalum cha kuzuia dawa za
kulevya Godfrey Nzowa ameiambia BBC kuwa Watu 12 wanashikiliwa kuhusiana
na shehena hiyo .Kamanda Nzowa amesema dawa hizo za kulevya zimekamatwa na Polisi wa doria baharini muda wa saa sita usiku wa kuamkia Jumanne zikisafirishwa katika Jahazi.

0 comments: