WAISLAMU WAENDELEA KUUWAWA KWA UMATI kwa mengi zaidi soma hapa ....by tuntu baby
Dunia ya leo jamani ni balaa huko myanmar..
Kundi la kutetea haki za binadamu la Fortify Rights limetangaza
kuwa askari usalama wa Myanmar wameua makumi ya Waislamu wa Rohingya
wakiwemo wanawake na watoto wadogo.Fortify Rights imetoa ushahidi wa watu walioshuhudia na nyaraka za kuaminika zinazothibitisha kuwa Waislamu wasiopungua 40 waliuawa kwa umati katika shambulizi lililofanywa na askari usalama wa serikali ya Myanmar tarehe 13 mwezi huu wa Januari kwenye jimbo la Rakhine. Kundi la Fortify Rights limesema idadi halisi ya Waislamu waliouawa katika shambulizi hilo yumkini ikawa kubwa zaidi na kwamba serikali ya Myanmar inawazuia waandishi habari na mashirika ya kutetea haki za binadamu kuingia kwenye maeneo yanayoshambuliwa.
Umoja wa Mataifa na nchi kubwa duniani zimetaka kufanyike uchunguzi kuhusu mauaji hayo.
Maelfu ya Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar wameuawa, kubakwa na wengine wengi wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na hujuma zinazofanywa na Mabudha wenye misimamo mikali wakishirikiana na jeshi la serikali ya nchi hiyo.... by tuntu baby
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI......
0 comments: