Battlefield 3 multiplayer review

Lorem ipsum dolor sit amet, conscur adisng elit, sed do eiusmod tempor iniunt ut labore et dolore mana aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exetation ullco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo coequat. Duis aute irure dolor

A Bathing Ape 2011 Winter Collection

Lorem ipsum dolor sit amet, conscur adisng elit, sed do eiusmod tempor iniunt ut labore et dolore mana aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exetation ullco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo coequat. Duis aute irure dolor

Diablo 3 beta gameplay video

Lorem ipsum dolor sit amet, conscur adisng elit, sed do eiusmod tempor iniunt ut labore et dolore mana aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exetation ullco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo coequat. Duis aute irure dolor

Killer Elite movie review

Lorem ipsum dolor sit amet, conscur adisng elit, sed do eiusmod tempor iniunt ut labore et dolore mana aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exetation ullco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo coequat. Duis aute irure dolor

                                      http://assets.audiomack.com/bongofive/6d64a77b571cc0f1998ef388b2724bff-275-275.jpeg 
<iframe src="http://www.hulkshare.com/embed.php?fn=spx2gvtzjbi8" scrolling="no" frameborder="0" width="100%" height="160px"></iframe>
by nasanyo fortnine
Vikosi vya zima moto vya Libya vinapambana kujaribu kuuzima moto baada ya kombora la roketi kulipua  
tanki la kuhifadhia mafuta wakati wa mapigano kati ya makundi mawili yanayohasimiana katika mji mkuu Tripoli. Tanki hilo ni miongoni mwa matanki yanayomilikiwa na Kampuni ya mafuta ya serikali ya Libya yenye lita milioni sita za mafuta.
Msemaji wa Kampuni hiyo Mohamed Al-Hariri amesema iwapo moto huo utasambaa kwenye matanki mengine ya karibu huenda ukasababisha madhara makubwa katika eneo lenye upana wa kilomita tano.
Serikali ya muda ya Libya imetaka ustishaji wa mapigano katika eneo hilo la maafa ili kuruhusu vikosi vya zima moto kufanya kazi yao bila kuingiliwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Stephen Wassira akizungumza kwenye mdahalo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema) Tundu Lissu na katikati ni Mwenyekiti wa CUF,  Profesa Ibrahim Lipumba
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira akiwakilisha CCM, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, jana walitoana jasho katika mdahalo wa Katiba ulioandaliwa na East African Business and Media Institute.
Mdahalo huo uliohudhuriwa na watazamaji wapatao 500, ulikuwa na mada inayosema: ‘Nani anakwamisha Upatikanaji wa Katiba Mpya.’ Kila upande ulitumia fursa hiyo kutupa shutuma kwa mwingine huku jazba na kelele vikitawala miongoni mwa waliohudhuria.
Hata hivyo, suala la muundano wa serikali ndiyo uliochukua nafasi kubwa katika mdahalo huo huku Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ukiishutumu Serikali ya CCM kuwa ndiyo kikwazo cha upatikanaji wa Katiba Mpya nayo ikitupa mpira huo kwa Ukawa kwa kitendo chake cha kutoka katika Bunge Maalumu la Katiba.
Profesa Lipumba alisema wahafidhina wa CCM ndiyo waliomshauri Rais Jakaya Kikwete abadilike kimsimamo kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya.
“Rais Kikwete alikuwa na nia njema kabisa kuhusu Katiba Mpya lakini wahafidhina wa CCM wanaopenda madaraka walipoona muundo wa serikali tatu wakambana naye akabadilisha msimamo, tunamwomba abadilike, nchi hii ni yetu sote ili tupate katiba ya wananchi,” alisema.
Lissu aliongeza kwa kusema kuwa anayekwamisha upatikanaji wa Katiba Mpya ni CCM ambao wanaweka maoni yao badala ya kujadili rasimu iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ndiyo maoni ya wananchi.
“Hatuwezi kurudi kwenye Bunge Maalumu la Katiba kwenda kujadili rasimu ya CCM kwa sababu wanaonyesha hawana nia ya Katiba Mpya, bali wanataka kuwadanganya Watanzania, watawadanganya wananchi kwa kuleta Katiba ileile ila ikiwa na rangi tofauti,” alisema huku akishangiliwa.
Alisema Ukawa hawawezi kushiriki katika udanganyifu wa aina hiyo na kwamba wameamua kuwaachia CCM ili wananchi waweze kuwahukumu kwa uovu watakaoufanya.
Alisema kati ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba katika Kundi la 201, wajumbe 166 ni wana CCM walioteuliwa ili kuongeza idadi ya watu.
“Humo kuna viongozi wa dini mashehe na maaskofu na waganga wa kienyeji ambao ni wana CCM ili wapitishe Katiba yenye masilahi yao binafsi,” alisema.
Hata hivyo, Wassira alisema hoja za Ukawa hazina mashiko na kumtaka Lissu kuwaomba radhi masheikh na maaskofu kwa kuwa hawakuteuliwa na Rais kutokana na kuwa wanachama wa CCM, bali ni mapendekezo ya taasisi wanazozitumikia.
“Namwomba Tundu Lissu akawaombe radhi masheikh na maaskofu kwa sababu kundi hili liliteuliwa kutokana na mapendekezo ya wahusika wenyewe pasipo shinikizo la Rais. Hapakuwa na uwezekano wa Rais kuwatambua wana CCM ili awateue wanaofaa. Kama ana ugomvi na Kingunge Ngombale Mwilu aseme.”
Matukio ya wazazi kuzuia watoto wao wa kike kuendelea na masomo yameendelea kushamiri licha ya serikali kukemea tabia hiyo, ambapo jijini Dar es Salaam mama mmoja anadaiwa kumzuia mtoto wake aliyefaulu kuingia kidato cha tano, kwenda shule.

Mwanafunzi huyo (Jina linahifadhiwa) anayeishi Mbagala Misheni  amefaulu kujiunga na Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa  ameshindwa kuhudhuria masomo kutokana na kudai kupigwa na mama yake aliyemtaja kwa jina la Yvonne Haule akimzuia kuendelea na masomo.


Akizungumza katika Ofisi ya Ustawi wa Jamii Manispaa ya Temeke, alikohifadhiwa msichana huyo, alisema mama yake amekuwa akimnyanyasa tangu wakati anasoma Shule ya Sekondari ya JKT Mgulani.


Alisema alimaliza kidato cha nne mwaka jana na kufaulu kwa alama ya daraja la tatu pointi 26 na kuchaguliwa kwenda kujiunga shule ya Benjamini Mkapa.


"Nilifurahi niliposikia nimefaulu kwenda kidato cha tano, lakini nilipomwambia mama hakuonyesha kufurahi, badala yake alisema hana huwezo wa kunisomesha," alisema binti hiyo.


"Niliwaza sana kwa nini mama ananifanyia mambo hayo ikiwa mimi ni mwanawe, nikijaribu kumuomba ananipiga sana na kunifungia mlango ili nisiingine ndani ya nyumba yake."


Kwa mujibu wa binti huyo,  mama yake alimzaa akiwa na umri mdogo na alilelewa na upande wa baba yake nchini Uganda, huko alisomeshwa hadi darasa la saba kabla ya kuhamia Tanzania mwaka 2009 akimfuata mama yake.


AJARIBU KUJIKWAMUA

Alisema katika jitihada ya kutafuta ada ya shule baada ya mama yake kugoma kumlipia, alitafuta kazi katika kampuni moja ya uuzaji wa vifaa vya nyumbani, hata hivyo hakuweza kujinasua baada ya kutolipwa pesa za mshahara.

Alipoona hakuna dalili ya kupata mshahara, aliamua kuondoka na baadhi ya vyombo vya kampuni ili kushinikiza alipwe kitu ambacho kilisababisha akamatwe na kuwekwa rumande kwa siku mbili.


"Nilipotoka rumande nilikwenda kwa mama kumuomba abadilishe mawazo yake, lakini hakuonyesha kunijali alizidi kusema hatatoa pesa zake kwani hata yeye ameishia kidato cha nne na anaendelea kuishi," alisema.


Hata hivyo, katika kutafuta njia ya kuondokana na tatizo hilo, alijaribu kupita katika ofisi mbalimbali za serikali, ambako huko wafanyakazi walimchangia pesa za ada na baadhi ya vifaa vya shule.


UTATA WAIBUKA

Kitendo cha binti huyo kuchangiwa pesa za kulipia ada ya shule, kilionekana kumkera mama yake kiasi ambacho kilimfanya apigwe na kutakiwa amtaje mtu aliyetoa pesa hizo.
Alipoona kipigo kinazidi, alikimbilia Ofisi ya Mtaa wa Bugud, na kufikishwa katika ofisi za Ustawi wa Jamii.

Afisa Mtendaji wa mtaa huo, Ruth Tete, alikiri kupokea malalamiko hayo na kueleza kwamba hata yeye ameshangazwa na hatua aliyochukua mwanamke huyo kumpiga mtoto wake na kumzuia kwenda shule.


"Tulijaribu kuwahoji wote wawili, lakini mama mzazi aling'ang'ania hawezi kumruhusu mwanawe kwenda shule hadi hapo atakapotajiwa mtu aliyetoa pesa za ada," alisema Tete.


MAMA AZUNGUMZA

Akizungumza kwa njia ya simu ya mkononi, Yvonne Haule, alisema kwa masikitiko kwamba mtoto wake ana tabia ya kuzusha maneno na kwamba ana ujeuri iliovuka mipaka kiasi ambacho anadiriki kumpiga pale anapomuonya.

Alisema yeye kama mzazi ana haki ya kumuonya mtoto pale anapoona anakwenda kinyume, lakini kwa binti yake huyo hataki kusikia jambo lolote kutoka kwake.


Alisema amemsomesha binti yake kwa gharama kubwa ambapo alikuwa akilipa ada ya Sh. 700,000 kila mwaka, hivyo anaposikia hataki kulipa ada kwa shule ya serikali anashangaa.


'Mzazi gani anayechukizwa na mtoto wake kufaulu, huo ni uwendawazimu, lakini huyu mtoto wangu anataka watu waamini mimi ni mzazi wa ajabu kabisa, ukweli ninampenda sana mwanangu lakini tabia zake zimekuwa za ajabu siwezi kuzielezea," alisema Yvonne.


Alifafanua kwamba, hata hiyo kazi ya kuuza vyombo alimtafutia wakati anasubiri majibu ili asiingie kwenye makundi mabaya.


Baada ya kupata kazi hiyo, tabia yake ilizidi kubadilika na kuanza kutorudi nyumbani kwao na anapoulizwa anakuwa mkali.


"Kitu cha kusikitisha mwanangu amefikia hatua hadi kutangaza kwamba eti namuonea wivu kwa kuwa amefaulu, inaniuma sana kibaya zaidi sasa hivi akiniona ananisonya na kunitemea mate," alisema kwa sauti ya kilio.


Hata hivyo anasema anamuachia Mungu suala hilo kwani yeye ndiye anafahamu kama anamfanyia vitendo vya unyanyasi mtoto wake.


Kauli ya mama huyo iliungwa mkono na mjumbe wa eneo hilo, Mzee Kabisa, ambaye alisema mara kadhaa alimuita binti huyo kwa ajili ya kumsihi asimdharau mama yake hadi kufikia hatua ya kupigana.


Mjumbe huyo alisema anachofahamu yeye Yvonne, alikuwa akijitahidi kumrekebisha mwanawe, lakini ameshindwa baada ya kila mara kuibuka vurugu.


"Kinachotokea hapa ni ushindani kati ya mtoto na mama yake, huyu binti amekuwa hamuheshimu mama yake na hata kesi zao nilikuwa nazisikiliza mara nyingi kabla ya kuhamia serikali za mita.


SERIKALI YAMSHIKILIA MTOTO

Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii wa Manispaa hiyo, Sultani Mziray, alipozungumza alisema wanaendelea kumshikilia mtoto huyo hadi hapo hatua mbalimbali za kuhakikisha anaanza masomo itakapochukuliwa.

Alisema tayari wameshamuhoji mama anayetuhumiwa kufanya vitendo hivyo wakati wanasubiri hatua zingine kuchukuliwa.


Copyright © 2014 NASANYO BLOG